Tuesday 20 August 2013

Keri Hilson akiri kumkubali Mr Flavour wa Nigeria

Mwanamuziki wa kimarekani, Keri Hilson amekiri kuwa jamaa wa kinaigeria, Flavour N'abania maarufu kama Mr. Flavour ni miongoni mwa wakali anaowazimia kinoma noma toka barani Afrika. Amesema anauzimia sana wimbo wake wa "Ashawo" japo haelewi maana yake. Keri ameshindwa kutoa maana ya jina la wimbo huo "Ashawo" kwa fans wake, kwa lugha ya kinaigeria ina maana ya "Whore".
Udhibitisho huo wa kumkubali mkali huyo kupitia kibao chake hicho cha "Ashawo", Keri Hilson aliandika  kupitia ukurasa wake wa twitter akionesha kama anaimba wimbo huo.

No comments:

Post a Comment