Wednesday 28 August 2013

Fat Joe jela kwa kukwepa kulipa kodi

Cartagena a.k.a Fat Joe au Joe Carta kama anavyopenda kujiita, Jumatatu ya wiki hii kwa mujibu wa wakili wake alisema kuwa mtu mzima Fat Joe alikiri Desemba 2012 kwa kushindwa kulipa kodi ya zaidi ya dola milioni 1 ya mapato ya mwaka 2007 na mwaka 2008.
Kwa kosa hilo atalazimika kulipa faini ya dola za kimarekani 15000 chini ya uangalizi mkubwa utaotolewa na mahakama ya jimbo la MIAMI, na itapaswa kulipwa ndani ya miezi minne ijayo kuanzia mwezi huu.

Joe amelazimika kuwahi kujiripoti kwa kuhofia uamuzi utaofanywa na mahakama ya jimbo hilo baada ya miezi minne juu ya wakwepa kodi

Msanii huyo ambaye alishafanya vizuri kwa kufikia mauzo ya platinum baada ya wimbo wake wa "WHAT'S LUV" kuingia kwenye chati ya Billboard nakusumbua kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment