Friday 5 July 2013

Yanga yatwaa million 90

http://www.zenjydar.co.uk/2009months/200901/images/yanga.JPG
Dar es Salaam. Mabingwa Yanga, usiku wa kumkia jana walitawala sherehe za kutoka zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu Bara, baada ya kuondoka na Sh90 milioni, huku wapinzani wao, Simba wakishindwa kutokea katika hafla hiyo kwenye Hotel ya Double Tree Masaki, Dar es Salaam.

Yanga ilitwaa Sh70 milioni baada ya kuibuka bingwa wa Ligi Kuu msimu uliomalizika, ikaongeza Sh15 milioni kama timu yenye nidhamu, huku beki wake mahiri, Kelvin Yondan akilamba Sh5 milioni kama mchezaji bora na kufanya jumla ya fedha zote kuwa 90 milioni.

Simba iliyomaliza katika nafasi ya tatu, ilistahili kupokea Sh20 milioni, lakini hakuna kiongozi wa klabu hiyo aliyekuja kushiriki kwenye sherehe hizo.

Taarifa za baadaye kutoka Simba zilidai kuwa, siku ya sherehe hiyo viongozi walikuwa kwenye mkutano hivyo kushindwa kufika. Awali, Yanga iliwahi pia kutangaza kutoshiriki sherehe hizo kabla ya kubadilisha uamuzi.

Masau Bwire, msemaji wa Timu za Majeshi, alisema walishindwa kushiriki kwenye hafla hiyo kwa sababu, siku hiyo walikuwa wakihazimisha siku ya kuanzishwa kwa majeshi na hawakuwa na taarifa za wachezaji wao kupata tuzo.

Sherehe hizo hazikuwa na ‘mashamsham’ kama ilivyotarajiwa, kwani mbali na Yanga timu zingine zilizohudhuria ni Azam, Kagera Sugar, na African Lyon, huku pia kukiwa na idadi ndogo ya waalikwa.

Kwa kumaliza nafasi ya pili, Azam walizoa Sh35 milioni, huku mshambuliaji wake Kipre Tcheche akiondoka na Sh5 milioni kama mfungaji bora.

Mwamuzi Simon Mbelwa alilamba Sh7.5 milioni kama mwamuzi bora wa mwaka, na zawadi ya Kocha bora Sh7.5 milioni ilikwenda kwa Abdallah Kibadeni.

Kipa bora ni David Burhani (Prisons), mchezaji mwenye nidhamu Fuli Maganga (Mgambo) kila mmoja alipata Sh5 milioni.

Kwa upande wa timu za vijana U20, walioibuka kidedea ni Abdurahaman Musa (JKT Ruvu), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting) Chande Magoja, Tom Kavishe (Mgambo) Hamis Saleh (Oljoro) na Rajabu Mohamed (Mtibwa) kila mmoja amepata kitita cha Sh1 milioni.

Naye Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo, alizitaka klabu kufuta utamaduni wa kushabikiwa migogoro mara kwa mara kwa vile mambo hayo hayana nafasi katika kukuza na kuendeleza michezo nchini 

No comments:

Post a Comment