Sakata
la usajili la mshambuliaji WAYNE Rooney jana usiku lilitishia kuivunja
familia yake kwa sababu mke wake Coleen hataki kuhamia nje ya nchi
hiyo...
Man United jana ilikataa ofa inayotajwa kuwa £20million
kutoka Chelsea, mahala ambapo mshambuliaji huyo inasemekana yupo radhi
kwenda kwa kuwa Coleen, 27, ataendelea kuwa karibu na wazazi wanaoishi
huko Liverpool.
Lakini United wanaonekana hawapo tayari
kuwauzia silaha wapinzani wao wa moja kwa moja ndani ya ligi kuu ya
England - hivyo kufanya kuwepo na uwezekano mkubwa wa uhamisho wa kwenda
Paris Saint-Germain kufanikiwa kama Moyes akiamua kumuuza Rooney.
Chanzo kimoja cha habari kilisema: “Suala hili la uhamisho wa Rooney
linasababisha hali tete baina ya Wayne na Coleen. Hawataki kuhamia nje
ya nchi. Lakini ikiwa hatashindwa kuhamia Chelsea basi mambo yatazidi
kuwa magumu kwao.
“Chaguo la kwanza la Wayne ni Chelsea kwa sababu wakihamia kusini mwa nchi bado wataendelea kuwa karibu na Liverpool wakiendesha masaa kadhaa kwenda mahala wazazi wao wanapoishi.
“Lakini United wamesema kwamba, ikiwa watamuuza - itakuwa ni kwa klabu ya nje tu, hivyo PSG wanaweza wakarudi na ofa nzuri.
"Coleen hataki kabisa kwenda Ufaransa kwa sababu anadhani ni mbali sana na ilipo familia yake, ambao wanamsaidia sana katika kulea wanae Kai na Klay.
"Hivyo ikiwa atauzwa, Wayne itabidi atumie ndege binafsi kutoka Paris-Liverpool, au aende kuishi mwenyewe hotelini.”

Mchana wa jana mke wa Rooney, Coleen alijikuta tena kwenye majibizano
makali na baadhi ya mashabiki kwenye mtandao wa Twitter ambao walikuwa
wakimtumia meseji ampelekee Rooney kuhusu suala la uhamisho wake - hali
ambayo inazidi kuleta hali tete.
CHANZO: SHAFFIHDAUDA.COM
No comments:
Post a Comment