Sunday 21 July 2013

Shilole ampania Sintah kumpa kichapo

Msanii wa kike wa filamu na pia ni mwanamuziki wa Bongo Freva, Zuwena Mohamed maarufu kama ‘Shilole’ ametangaza bifu kwa msanii mwenzake wa filamu na mtangazaji wa luninga, Christina John maarufu kama ‘ Sintah’ kuwa popote atakapomkuta lazima amchape kwa kipigo ambacho hatasahau katika maisha yake...
Shilole  ametoa kauli hiyo kufuatia kuandikwa na mwanadada huyo katika mtandao wake akimbeza kwa kejeli. .
“Ni kweli sisi wanawake hatupendani na kuwa na wivu wa kijinga, mtu anakurupuka anakotoka bila hata kufanya utafiti na kunibeza eti sina uwezo wa kuimba na JLO (Jenifer Lopez) ...
"Kuna mtu aliyetegemea mimi kwenda kufanya show Marekeni! Sasa ninachomwambia ninamtafuta nikikutana naye nimtapa kipigo cha Mbwa mwizi,”aliongea kwa hasira Shilole.

Katika mtandao wake Sintah aliandika kwa kusema Shilole ni sawa na mtu anayeota ndoto za mchana, na kumkejeli kwa kusema kuwa aendelee kuota anaweza baadae kurudi katika hali yake...
Shilole anasema kuwa hajawahi kumuona mwanamke mwenye roho dhaifu kama Sintah, anajifanya anambabaikia Jlo wakati hata hajulikani....

“Mimi sikuwa nimeenda Marekani kwa ajili ya kuomba kumshirikisha J-lo kuimba naye,  lakini baada ya meneja wake kuja kuniona na kumpelekea video za muziki wangu  JLO alikubali kufanya kazi na mimi...


"Ilitakiwa nionane naye siku ya Jumapili lakini ndio siku niliyoondoka na ninarudi huko kwa ajili ya kazi hiyo, sijui nikifanya naye kazi atajificha wapi?,” alisema Shilole.

Shilole anasema Mungu ni mkubwa hata kama kuna mtu anayemchukia kwa mafanikio yake bado Mungu ana nafasi kubwa kuwazima watu wenye roho mbaya wivu kama Sintah ambaye anaonekana yupo tayari kwa ajili ya kuwaombea matatizo watu wanaojituma kwa ajili ya kuendesha maisha yao.  

No comments:

Post a Comment