Sunday 28 July 2013

Mtanzania Omary Kimweri amtwanga M'australia "K-O"

BONDIA Mtanzania Omari Kimweri  'Lion Boy' anaefanya shughuli zake nchini  Australia amendelea kutamba katika nchi hiyo baada ya jana kumtwanga kwa  "KO" ya round ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand   ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangia angie katika ngumi za kulipwa akiwa nchini humo .


Bondia huyo ambaye anaitangaza vema nchi ya Tanzania Kimataifa ameaidi kuwa ataenderea kutoa vipigo kwa mabondia  mbalimbali  pindi wakutanapo ulingoni .


Kimweri aliezaliwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mwaka 1982 amekuwa gumzo nchini humo kwa kuonesha mchezo mzuri unaowavutia raia wengi wa Australia na kuweza kuwa bondia namba moja katika nchi hiyo uku katika Dunia akishikilia nafasi ya 52 katika mabondia 450 duniani wenye uzito wa light flyweight


Anasema lengo lake kubwa ni kuukamata ubingwa unaotambulika kimataifa Duniani wa WBA World light flyweight title unaoshikiliwa na bingwa namba moja Duniani ,Roman Gonzalez na IBF light flyweight title   unaoshikiliwa na  John Riel Casimero wa  Philippines ambao wananiumiza kichwa kwa sasa kwani ngumi ulimwengu mzima ni zile zile ila tunazidiana maarifa

Bondia huyo anaefanya shughuli zake za masumbwi nchini Australia ana mpango wa kuja kuwekeza nchini Tanzania mchezo wa masumbwi ili ukuwe hapa ambapo atafanya kila jitiadi ili mchezo wa masumbwi uweze kusonga mbele nchini.
CHANZO: www.superdboxingcoach.blogspot.com

No comments:

Post a Comment