Sunday 21 July 2013

Kanye West ampiga mpiga picha

Rapa na pia mtayarishaji wa muziki nchini Marekani, Kanye Omary West ijumaa ya wiki hii ameripotiwa kumpiga mpiga picha wa Los Angles, Marekani wakati akiwa amewasili katika uwanja wa ndege wa jijini hapo (Los Angles International Airport).

Kanye ambaye ni baba wa mtoto wa mwanamitindo Kim Kardashian, alifanya tukio hilo la kumtwanga mpiga picha huyo na kukimbilia kwenye gari akiwa na walinzi (Bodyguard) wake na kusepa katika eneo hilo.

Hata ivyo imeripotiwa kuwa mpiga picha huyo baada ya kupewa kichapo hico alipelekwa hospitali na kisha akafungua kesi na hadi sasa kesi iko mahakamani. Kesi hiyo yenye madai ya kumkaba mpiga picha huyo, ilihamishiwa kwenye mahakama kuu ya jiji hapo (Los Angeles) kwenye kitengo cha mashtaka kama hayo ya ukabaji/uporaji.

Kanye ambaye alishawahi kuzinguana na wasanii wenzake kama Taylor Swift na Pink mwaka 2009, hajatoa sababu zozote za kuishawishi mahakama kwanini alifanya kitendo hicho cha kumdunda mpiga picha huyo.

Kwa mujibu wa msemaji/mtoa taarifa wa tukio hilo aliyekuwepo katika eneo hilo la tukio la Los Angeles International Airport, amesema haikuweza kufahamika kama huyo mpiga picha ni mwandishi wa kituo kipi cha utangazaji au ni raia wa kawaida kwa kuwa hakuwa na utambulisho wowote.

Kanye hakuweza sema chochote baada ya kutafutwa na waandishi kuhusiana na tukio hilo nakusema, "Don't talk to me, don't talk to me please!!"

No comments: