Friday 12 July 2013

Kampuni yamlipa Clinton $700,000 kuongea kwenye tafrija yao

Kampuni moja ya nchini Nigeria (jina limehifadhiwa), imelazimika kumlipa aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton kiasi kikubwa cha fedha ili aweze kuzungumza kwenye tafrija iliyokuwa imeandaliwa na kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari (The New York Times) kimeripoti kuwa kampuni hiyo ambayo hawakuibainisha imemlipa rais huyo kiasi cha Dollar za Kimarekani 700,000 ambazo ni billions nyingi kwa pesa ya madafu ya hapa Bongo.

Mbali na kualikwa huko na hiyo kampuni, Clinton amekuwa akitembelea Nigeria mara nyingi tu, na kwa mujibu wa chanzo hicho, wiki mbili zilizopita Clinton alialikwa kwenye uzinduzi wa Ecko Atlantic City na Thisday Awards kama mgeni mzungumzaji (guest speaker).

Pia kwa mujibu wa magazeti ya kila siku ya nchini Marekani yamesharipoti kuwa rais huyo ameingiza kiasi cha pesa ambazo ni Dollar za kimarekani 17million kwa mwaka jana peke yake kwa ajili ya kutoa hotuba tu kwenye shughuli mbalimbali alizoalikwa, japo chanzo hicho hakikuweka bayana kwamba ni lini amelipwa kiasi hicho cha pesa. Hillary Clinton, mke wa rais huyo mstaafu naye anatarajiwa kulipwa kiasi cha $200,000 mwezi ujao kwa kualikwa kwenye mkutano wa Global Business Travel Association huko San Diego, ambapo mumewe (Bill Clinton) alipokea kiasi cha $250,000 mwezi June.

Baadhi ya wafanyabiashara ambao walimualika Bill Clinton kuja Nigeria akiwemo na Nduka Obaigbena, publisher wa gazeti la ThisDay ambalo wafanyakazi/waajiriwa wake Mei 2013 walilalamika kutolipwa mishahara yao kwa miezi kadhaa.

Yasemekana Nigeria ni nchi ya pili kwa Utajiri barani Afrika, lakini kwa mujibu wa National Bureau of Statistics inasema kwa mwaka jana 100 million zimepungua toka kwenye 160 million kwa wanaigeria wanaoishi kwenye mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment