Sunday 21 July 2013

Jamaa atimua mbio akiwa uchi

Jamaa aliyefahamika kwa jina la Wati Holmwood, mwenye umri wa miaka 33, mwenyeji wa Sydney aliamua kuingia ndani ya uwanja wa ANZ na kuanza kucheza huku akiwa uchi kama alivyozaliwa.
Jamaa huyo mwenye mwili kiasi cha kutosha alikimbizwa na kudakwa na walinzi katka kile kilichochukua muda wa dakika kama moja kuuzunguka uwanjani.
Holmwood alisema alitaka kukimbia umbali wa kilometa 10 akiwa kwenye hali hiyo mara baada ya kutolewa nje ya uwanja.
Inafahamika kwamba Holmwood aliupaka mwili wake mafuta ili kuwe na ugumu wa kumshika pale atakapokamatwa na vyombo husika akiwa kwenye zoezi hilo.
Juhudi zake zilimkuta akiishia hospitali ya Auburn iliyopo ndani ya jiji la Sydney huku gazeti la Telegraph likitaarifu alionekana akiwa "amechanganyikiwa na hajielewi" baada ya kuamka na kujikuta kwenye hali aliyokuwa nayo.

No comments:

Post a Comment