Friday 12 July 2013

Halle Berry anatarajia kuolewa tena kwa mara ya nne

Berry na Martinez

 Berry na Gabriel Aubry

 Berry na Eric Benet

 Berry na David Justice

Actress mashuhuli wa Marekani, Halle Berry ametangaza kufunga ndoa kwa mara nyingine tena na mchumba wake, Oliver Martinez wiki hii.

Berry alishawahi kuuambia ulimwengu kuwa hana mpango na hatarajii kuolewa tena, lakini mwanzoni mwa wiki hii amesema ameshangazwa na kitendo alichofanyiwa na mchumba wake huyo ambae ni muigizaji wa Ufaransa kwa kumvisha pete. Pia alishawahi kutoa maneno yenye kejeri kabla ya kuvishwa pete hiyo ya uchumba na mchumba wake Oliver, "who knew? I swore it off, right? Never say never, people!"

Berry amekaa kwa muda tangu kuachika March, 2012. Hivyo kama ataolewa tena hii itakuwa ni mara yake ya nne kwa Berry kuolewa, baada ya kuolewa na David Justice mwaka 1991, 2001 pia aliolewa na muimbaji Eric Benet.

Muigizaji huyo, Oliver Martinez amesema ndoa yao itakuwa ni ndogo tu na yakawaida sana ila hayuko tayari kusema walichopanga kufanyikia kwa ndoa hiyo.

Berry na Martinez wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza mapema mwaka huu, na mimba ya mtoto huyo mtarajiwa iko open kwa muigizaji huyo nyota, Halle Berry.

No comments:

Post a Comment