Sunday 2 June 2013

Kibaka aliyechomwa moto Mbagala

Kibaka mmoja amejikuta akiyaaga maisha ya uraiani baada ya kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali....
Tukio hili limetokea maeneo ya mbagala charambe mida ya saa sita mchana baada ya kibaka huyu kuingia ndani ya nyumba ya mtu na kuiba begi...
Taarifa zinaeleza kwamba, raia mwema ambaye ni mkazi wa nyumba hiyo alisahau kufunga mlango na kwenda kwa jirani...Alipotoka tu, Kibaka huyo alizama ndani na kuchukua begi la nguo taratiiibu kama lake!
Hakuridhika na begi, alivyotazama pembeni aliona kuna simu. Bila kupoteza muda, kibaka huyo aliihifadhi mfukoni ..
Balaa liliazanza wakati anajiandaa kutoka...Alipofika mlangoni, kibaka huyo alikutana na mwenye nyumba uso kwa uso.....!!!
SINEMA ILIANZIA HAPO!!!!! Watu mwiziii... mwiziiii mwiziiiiiiiiiii....!!!!!
Kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu, jamaa huyo alibahatika kujisweka ndani jumba bovu lililoko uchochoroni na kuinusuru roho yake....
Raia wenye hasira kali hawakumuona wakapita, Kufika mbele kidogo walikata tamaa. Wakati wanarudi nyumbani kwao mara ghafla jamaa akakurupuka na kuchomoka kwenye dirisha la lile jengo bovu alikokuwa amejificha....
Harakati zikaanza upyaaaaaa!!!!! YAAAANI...!! Kibaka hakuchukua raundi akatiwa mikononi...

No comments:

Post a Comment