Tuesday 25 June 2013

Janeth Jackson aamua kuslim

Dada wa aliyekuwa mfalme wa muziki wa Pop duniani (Michael Jackson), Janeth Jackson ameamua kuwa muislam baada ya kile kinachosadikiwa kuwa ameolewa na mume wa kiislam na kuamua kubadili dini na kuwa muislam.

Janeth ameamua kuachana na muziki aliokuwa akiutumikia kwa takribani ya miaka 30 na kuamua kumgeukia Mungu. Kwa US imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya mastaa kuamua kuslim na kuwa waislam, kwani tuliona msanii Loon aliamua kuwa muislam na kuachana kabisa na mambo ya muziki, pia tukaona kwa mfalme wa ndondi, Mike Tyson nae aliamua kuslim nakuwa muislam. Hivyo si ajabu sana kwa uamuzi aliouchukua mwanadada huyo.

No comments:

Post a Comment