Thursday 2 May 2013

Tujaribu kikuza lugha yetu ya kiswahili

Tunafahamu kwamba Tanzania ina zaidi ya makabila 120, na makabila yote hayo yanatumia lugha zao za asili kama njia ya mawasiliano kwa namna moja ama nyingine. Tatizo linakuja pale wanapotumia lugha zao za asili hata mashuleni katika kufundishia masomo mbalimbali. Hili naweza sema ni tatizo kubwa kwa maana inakwamisha ukuzaji wa lugha ya kiswahili na hasa kuwafanya washindwe kabisa kujifunza lugha za kimataifa kama Kiingereza.

Shule ya sekondari Chagaa iliyopo wilayani Kondoa katika mkoa wa Dodoma imeamua kupambana na tatizo hilo kwa kuweka baadhi ya njia kuhakikisha wanamaliza tatizo la kutumika kwa lugha ya asili shuleni hapo kwa maana wanafunzi wa shuleni hapo utumia sana lugha ya kirangi zaidi kuliko lugha za kiswahili na kiingereza.
Hiki kibao kipo kwenye mti shuleni hapo

No comments:

Post a Comment