Monday 13 May 2013

Diva aweka wazi penzi lake kwa Prezzo


Diva Lovenes

Huddah Morone
Kwa sasa hakuna siri tena kuwa mtangazaji wa clouds, Loveness a.k.a Diva na Msanii kutoka nchini Kenya CMB Prezzo ni wapenzi. Uvumi huu ulianzakukolea mwanzoni mwa wiki iliyopita ambapo ilisikika kuwa Diva amemkolea Prezzo baada ya mtu mzima Prezzo kutua bongo na kuchill masiku kadhaa ndipo wakanasana. Kwa mahojiano yaliyofanywa na Soud Brown C.E.O wa Makorokocho Diva alitupilia mbali habari hizo na kusema si wapenzi zaidi ya kuwa washkaji tu, ila kwa upande wa Prezzo alisanuka na kudai kuwa yuko na plani za kufunga ndoa na Diva.

Basi story hizo zimethibitishwa na mtangazaji huyo "Diva" kupitia mtandao wa twitter na kutupia tweet ambazo zinaweka wazi kuwa yeye na Prezzo ni wapenzi na sio siri tena.
Hata hivyo Diva amejikuta anaingia kwenye mabishano ya uhasama na model wa nchini Kenya "Huddah Monroe" a.k.a The Boss Lady ambaye inasemekana yeye na Prezzo walishawahi kuwa wapenzi. Uhasama huo umechukua uwanja mpana sana na kusababisha makundi mawili "Kenyans na Tanzanians" yaan kundi la watanzania wanaomsupport Diva na wakenya wanaomsupport Huddah Moroe.

No comments:

Post a Comment