Thursday 9 May 2013

Aunt Lulu:"kujiuza sasa basi"

Aunt Lulu enzi zake
Baada ya msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo maarufu kwa jina la ‘Aunty Lulu’ kunaswa akijiuza, sasa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha yake aliyokuwa akiishi zamani na kuwa na maisha mengine ya kimaadili.

Akiongea na chanzo cha habari hii, Aunt Lulu alifunguka kuwa kwa sasa ameamua kubadilika kwani kama ni starehe amefanya sana pamoja na uchafu mwingi ila kutokana na mtego wa kujiuza kumnasa na ushauri aliopewa na familia yake, amebadilika na sasa amegeukia kwenye ujasiriamali.

Aunt lulu ofisini kwake
Yaani kutokana na mtego wa kujiuza nimeamua kubadilika kwa sababu jamii ilinichukulia tofauti sana hivyo nikaamua kufanyia kazi ushauri wa familia yangu niliokuwa nikipewa kila siku lakini nikawa naukataa.

Kwa sasa nafanya ujasiriamali na ninafurahia maisha haya kuliko yale niliyokuwa nikiishi zamani. Aunty Lulu kwa sasa anamiliki duka la vipodozi na ni wakala wa kutoa na kuweka fedha kwa kupitia mitandao ya simu za mkononi maeneo ya Kinondoni Kanisani, DSM ambapo ndipo anashinda kwa sasa na kwa mujibu wake ameachana kabisa na kujiachia kwenye sehemu za starehe na kufanya mambo yasiyotakiwa katika jamii.

CHANZO: KISHYMBA BLOG

No comments:

Post a Comment