Saturday 6 April 2013

Sean Kingston aghailisha show baada ya promota kuzingua


Rapa wa marekani ambaye pia ni raia wa Jamaica aliyetamba na ngoma kama Beautiful, Me love, Face drop, Dutty Dutty akiwa na Nikki Minaj pia alisikika kuwa ameshafanya ngoma na msanii wa hapa Bongo (AY) japo bado hatujapata kuisikia wala kuiona kwenye kituo chochote cha redio au TV, hapa namzungumzia Sean Kingston au Sean Big kama anavyopenda kujiita.


Jana usiku kupitia ukurasa wake wa facebook mtu mzima Sean Kingston amefunguka kwa mashabiki wake walioko Miami yakuwa hatoweza kupiga show katika jiji hilo ambapo alitakiwa kufanya bonge la show ndani ya Central Broward Regional Park tarehe 7 April kutokana na kuzinguliwa na promoter wa show hiyo.

So, ameomba radhi kwa wadau na mashabiki wake kwa tukio hilo ambalo lipo juu ya uwezo wake na team control yake mzima...."Attention all my Ft. Lauderdale and Miami fans...I WILL NOT be at Central Broward Regional Park on April 7th! The promoter did not handle business. Sorry to all my fans and I hope to see you soon, but this was out of mine and my team's control" alisema hayo mtu mzima Kingston.

Amesema ameamua kutoa taarifa hizo mapema kwa kuwa na wasiwasi kwa wadau wake kuwa tayari wameshanunua tickets za show hiyo, so ili kuepusha usumbufu na hasara kwa mashabiki wake.

No comments:

Post a Comment