Tuesday, 30 April 2013

Mwanamke mwenye asili ya Afrika awa Waziri Italia

Mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Kiafrika aitwae Cécile Kyenge Kashetu kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amechaguliwa kuwa Waziri nchini Italia. Alizaliwa kijijini Kambove, mkoani Katanga, nchini DRC, August 28, 1964 na baadae aliolewa na Mwitaliano ambapo mpaka sasa ni Mama wa watoto wawili... Alihamia nchini Italia mwaka 1983 na kuchukua uraia... Alihitimu mafunzo yake ya Udaktari unaohusiana na madawa katika chuo cha Universita Cattolica del Sacro Cuore kilichopo Roma, baada ya kumaliza chuo makazi yake yalikuwa eneo moja liitwalo Castelfranco Emilia, Jimbo la Modena, mkoa wa Emilia- Romanga akiwa anaendelea na kazi yake ya udaktari... 
Akiwa kwenye majukumu yake
Mwaka 2004 alijiunga na mambo ya siasa katika chama cha PD yaani ''Partito Democratico'' na alipata nyadhifa mbalimbali mwaka 2010, lakini February mwaka huu ndio alichaguliwa kuwa Mbunge kupitia chama chake cha PD... Mwezi huu wa April 2013 ndipo mama huyu amechaguliwa kuwa Waziri anayehusika na mambo ya kigeni kwenye Serikali ya Enrico Letta... Hii ni sifa kubwa kwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Afrika kwa ujumla.

No comments: