Wednesday 24 April 2013

Mama yake Zitto avamiwa

Mama mzazi wa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, amenusurika kutekwa. Waliomvamia wamemtishia kumuua huku wakimtaka awape laptop,simu na mawasiliano yake mengine...


Habari zaidi magazeti ya leo;
Mtanzania na propaganda wamesema "mama yake Zitto alimwona kada wa chadema na anamfahamu yale yale ya baba yake Mtela Mwampamba, mtu amuonye tu Shida binti Salum ana heshima kwenye jamii asijiingize kwenye propaganda za kusaidia usaliti wa mwanane wa masalia, mama tulia kula vya mwanao pole pole dhambi ya uongo ni mauti , sasa hili dili litakufa kama lilivyokufa la video, pole mama habari ya leo ni liwale"
Quote By Zitto
Nimekuwa naulizwa kuhusu Habari za mama yangu Mzazi Bi. Shida kuvamiwa na kutishiwa bastola. Nawajibu watu Kwa ujumla kwamba

"Moja, mie sio msemaji wa familia. Ni basi tu katika watoto wa mama yetu mie najulikana zaidi na hivyo mama anaitwa Mama Zitto. Kwetu Kigoma haitwi hivyo, ama Ni mama Salum au mama Lulu.

Pili, hili Ni suala la polisi. Lipo polisi na linashughulikiwa na polisi. Nisingependa kulisemea wakati Ni suala linalochunguzwa na polisi. Mama yangu Ni mama wa kawaida wa kitanzania kama mama mwingine yeyote yule. Matukio ya namna hii yamezagaa nchi nzima. Hivyo suala lake litashughulikiwa kama yanavyoshughulikiwa masuala mengine yote ya Watanzania. Polisi wakimaliza uchunguzi wao naamini hatua mwafaka zitachukuliwa.

Ushauri- tuwe makini na "Agente provocatuers" au in English "provocation agents" nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata"

Nawatakia Kila la kheri katika kazi za ujenzi wa Taifa letu na kuimarisha Umoja na mshikamano wa Watanzania dhidi ya ufisadi, umasikini
na ugandamizaji.
Source: JamiiForums

No comments:

Post a Comment