Tuesday 16 April 2013

JB atangaza kugombea ubunge

JB a.k.a Bonge la bwana
Mwigizaji mahiri nchini hapa Tanzania, Jacob Stephen maarufu sana kama ''JB'' au Bonge la bwana kama anavyojiita, amesema yupo mguu sawa kuingia kwenye ulingo wa siasa kwa kugombea ubunge mwaka 2015...
Akizungumza na gazeti la ''Habari Leo'' jijini Dar es Salaam jumamosi iliyopita (taerehe 12/04), JB alisema ameamua kuweka wazi ndoto yake hiyo ya miaka mingi kwa nia ya kuwatumikia Watanzania...
JB alisema, hapa namnukuu: ''Nimeamua kuweka wazi kwamba, mwaka 2015 nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda mwafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii…"
Hata hivyo, JB hakuwa tayari kuanika ni jimbo gani atagombea alisema atatangaza baadaye licha ya kudai kwamba ni jimbo moja lenye upinzani mkali…
JB alisema: ''Nasisitiza nitagombea, lakini siwezi kuweka wazi ni jimbo gani, hilo nitaliongelea baadaye, ila ni kubwa lenye upinzani mkubwa kila wakati wa uchaguzi''…

No comments:

Post a Comment