Tuesday 30 April 2013

Jay Z ataja timu ya soccer anayoizimia

Hiphop star wa dunia, Rapper Jay Z kutoka nchini Marekani, alikua mmoja kati ya waliohudhuria mechi ya Arsenal na Manchester United iliyochezwa majuzi, mechi iliomalizika kwa sare ya 1-1 ambapo pembeni yake, Jay Z alikua na mwimbaji ambae ni Lead Singer wa Coldplay Chris Martin... 

Hii ni mara nyingine tena kwa Jay Z kuhudhuria mechi ambayo Arsenal inacheza, aliwahi kuhudhuria ya Man City vs Arsenal kwenye uwanja wa Etihad mwaka 2010 akiwa mgeni aliealikwa na Man City, ambapo baadaye ripoti za waandishi zilisema Jay Z ni shabiki wa Man City... Alipoongea na Jarida la Arsenal hiyo juzi, Jay Z alisema: ''Baada ya ile mechi naona kila mwandishi aliripoti kwamba mimi ni shabiki wa Man City, hapana!... Kila mmoja nchini hapa Uingereza anajua kabisa kwamba mimi ni shabiki wa Arsenal''...alifunguka hayo mwanamuziki huyo mkongwe mwenye kisu kirefu pia ni baba wa mtoto mmoja aliyebahatika kuzaa na mwanadadashost Beyonce mwenye kisu kirefu pia.

No comments:

Post a Comment