Wednesday 3 April 2013

gari aina ya spacial yaibiwa Dar

"Usiku wa jana Tarehe 01/04/2013 mida ya saa tano na nusu hivi (23:30 pm). Mtaa wa Goba Mbezi ya Tangi Bovu nyumbani Nimeibiwa Gari aina ya SPACIO number T 424 CHH NYEUSI" alisema jamaa aliyeibiwa gari hilo.
Ni majambazi waliokuwa wakifuatilia Gari kwa nyuma tangu Mitaa ya Samaki Mbezi beach mpaka gari ilipofika nyumbani kabisa getini ndipo walipotrack gari kwa kuja mbele na kuamulu Dereva ashuke na kulala chini kifudifudi, Wakiwa wameshikilia Bastora na Mapanga, waliingia nakuondoa Gari kisha kutokomea pasipojulikana.
Taarifa nimepeleka Kituo cha POLICE tayali so naomba msaada kwa watanzania wenzangu naamini sote ni ndugu na tunaupendo wa dhati kwa kila mmoja wetu, Atakae iona gari hii atoe taarifa kituo cha POLICE chochote karibu yake au apige simu number  
0713 302 823
0753 481 368

No comments:

Post a Comment