Monday 11 March 2013

sauti sol kuperform lagos


 SAUTI SOL
Kundi maarufu la muziki nchini Kenya Sauti Sol wanatarajia kusafiri kuelekea jijini Lagos nchini Nigeria kuipeperusha bendera ya Kenya katika tamasha la Inaugral Viewers’ Choice Awards litakalofanyika jumamosi hii nchini humo.

Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zitakuwa zikiburudishwa kupitia wanamuziki na bendi maarufu wakiwemo magwiji wa muziki barani Afrika Femi Kuti, Tiwa Savage, Chidinma na wengineo wengi.
Aidha Sauti Sol watapata nafasi ya kujumuika na nyota wengine wa filamu nchini Nigeria kama vile Chinedu Ikedieze, Genevieve Nnaji, Majid Michel, Omotola Jalade-Ekeinde, Rita Dominic na wengineo kibao watakokuwa wakishiriki katika utoaji wa tuzo hizo

No comments: