Jiji la Dar es salaam limekuwa na maafa yenye kuua takribani watu wengi sana kwa matukio ambayo hayana majibu kwa jamii na serikali kwa ujumla. Tunakumbuka mwaka 2002 kuna maafa yalitokea bahari ya Hindi yaliyojulikana kwa jina la "TSUNAMI" na kuua watu kadhaa wa jiji la Dar es salaam.
Mbali na tukio hilo likaja la mabomu ya Mbagala ambayo nayo yaliua watu wengi tu tena wasio hata na hatia, achana na hilo likaja la Gongo la Mboto pia wakafa wananchi wengi tu wasio na hatia....
athari za mabomu- gongo la mboto
Yote tisa...kumi la mafuriko yaliyoiwekea historia jiji la Dar es salaam kwa kuua watu zaidi ya 200 na kuwafanya baadhi ya wananchi wakose mahali pakuishi hadi leo.
athari za mafuriko - Dar(2011)
Leo hii majira ya saa tatu asubuhi yametokea maafa mengine yaliyoteketeza maisha ya watu waliokuwepo katika eneo hilo.
Baadhi ya viongozi na wanausalama wamefika eneo la tukio, pia rais
Jakaya Kikwete mchana huu ametembelea eneo lilipoanguka jengo hilo na
kuhimiza juhudi za uokoaji ziongozwe ili kuokoa maisha ya watu
wanasadikiwa kuwa wapata 60 waliofukikwa ndani ya Kifusi.Tayari askari
wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT) na lile la Wananchi(JWTZ) wapatao 500
wako eneo la tukio katika juhudi za uokoaji.
baadhi ya picha za tukio hilo
Mkuu
wa mkoa Said Meck Sadick akiwa na Rais Kikwete na Kamanda wa polisi
kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova, wakiwa wanaangalia jengo
lililo dondoka
hii ni taswira ya juu
juhudi za uokoaji zikiendelea
No comments:
Post a Comment