Monday 10 December 2012

ray c amtokea jk ikulu

JK and Ray C 
Mh.Raisi Kikwete akiwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati mwanamuziki huyo alipoenda kumtembelea Raisi na kumpa shukrani kwa kumsaidia kwenye matibabu ya juu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. 
Aidha Ray C alimueleza Raisi kwamba afya yake imeimarika na kwamba muda mfupi ujao atarudi kuendelea na kazi yake ya muziki. Kwa upande wa mama yake Ray C amemshukuru Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanae kwa kugharamia matibabu yote ya mwanae.
Mama yake mzazi Ray C (Margreth Mtweve)
JK, Ray C na dada wa Ray C (Sarah Mtweve)
source: baabkubwa magazine

No comments: