Monday 28 May 2012

YALIYOJILI MECHI YA BASKET MIPANGO VS UDOM

Jumapili (tar 27) Timu ya mipango ilichuana na timu ya Udom kwa kuwania kombe la ligi ya mkoa wa dodoma katika mpira wa kikapu. Timu ya UDOM iliibuka kinara baada ya kuichapa timu ya MIPANGO kwa vikapu 65 kwa 60. Mchezo ulikuwa wakusisimua kwa ushindani na upinzani uliokuwapo kati ya wahasimu hao. Mechi hiyo iliuzuliwa na diwani wa kata ya Mnadani Mh.Steven Masangia ndio alikuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo. Michuano hiyo ilijumuisha jumla ya Timu tisa zikiwemo MIPANGO, UDOM, CBE, DO Worrios,Dom Spurs, St.John, Don Bosco na Dom Spears. Timu ya CBE ndio iliyoshika nafasi ya nne baada ya kuchapwa na timu ya Dom spurs vikapu 56 kwa 34 na kuipa ushindi wa nafasi ya Tatu timu ya Dom spurs.
 timu ya mipango ikipata mawaidha toka kwa Kocha wao
Big Fish, kabla ya game kuanza
 timu ya UDOM ikipeana mawaidha kabla ya game
 muonekano wa uwanja (court)
 Timu zo zikiwa zimejipanga kwa kusalimiana na mgeni rasmi
 Mmoja wa mashabiki waliokuwa na mizuka kutoka chuo cha
MIPANGO
 Play-Maker wa UDOM (Ntandu) akichuana na Middle ya
 Mipango (Isack)
 Vijana wa UDOM wakijaribu kushambulia goli la Mipango
 Captain wa timu ya Mipango akipokea kombe la mshindi wa 2
Captain wa UDOM akipokea kombe la mshindi wa 1

No comments: