Tuesday 20 March 2012

KUTOKA FACEBOOK

SOMA KWA MAKINI SANA !!!
UMEFIKA NYUMBANI UNAKUTA BARUA YAMWANAO HII UNGEFANYAJE?
Baba na mama,ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye
karatasi niliyoiweka juu ya meza,naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida
kwenye maisha tunayoishi,najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndo nipo kidato cha kwanza,Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo
nyumbani,nimeto roka mana nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa
sababu mi ni kijana mwenyewe umri wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi
kibaya.tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano na binti mmoja aliyeitwa Rachel,mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenye chumba
alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000,msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na
ninampenda sana,amenifundi sha njia za kutafuta hela.Amenipangi a kazi ya kuuza
madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku anaenda kuuza mwili wake,basi
kila siku tunapata hela ya kutosha,huyu mchumba wangu ni msichana mwenye
bidii,kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye
chumbani kwa mda wa masaa 3.Msiwe na hofu,nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri,Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga mwilini,mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani,iwe kufanyanaye mazoezi ya viungo au kufanya kila anachotaka,si mnajua unapokuwa
na mgonjwa unakuwa naye karibu,ila mi pia sijihisi vizuri mana kila
saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea, nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa ameshajifungua, na nifuraha yangu mtamwona mjukuu wenu.Wazaziwangu sina la kuongeza kwaherini Mungu akipenda tutaonana. Baba na mama mi nipo chumbani kwangu, mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi,naomba iangalieni kama kuna makosa...

No comments: