Monday 26 March 2012

BIFU LA WASANII WA BONGOFLEVA

Nicki Mbishi na Bonta Maarifa kutoka Weusi
 Nicki Mbishi
Weusi
Baada ya Nicki Mbishi kutangaza rasmi kujitoa Lunduno, sasa asanuka na bifu la yeye na Weusi. Nicki Mbishi aliyefanya mahojihano na moja ya redio maarufu hapa bongo amesema, ameshangaa sana kuona Bonta kutangaza bifu nayeye. Kisa cha bifu hilo inasemekana kuwa wanagombania jina la CONSCIOUS ambalo linatumiwa na wasanii hao. Kwa mujibu wa Bonta anasema yeye ndio mwanzilishi wa jina hilo hivyo basi Nicki Mbishi anakopi jina hilo na kulitumia yeye. Mbali na malalamiko hayo yanayohusu jina la CONSCIOUS, Nicki Mbishi pia amelalamikiwa kuwapiga madongo wakali hao kutoka kundi la Weusi mfano, kuna mstari unasema: “iweje Nicki wa pili wakwanza hajulikani” hii inaweka wazi kuwa jamaa amediss Nicki wa pili kujiita hivyo.
Nicki Mbishi amesema “Kwakuwa wameamua kutangaza bifu basi acha liwe bifu kati yangu na hao wanao jiita weusi au waanzilishi wa Hip Hop Tanzania, kwanza hata KalaPina alisema kwenye tamasha la Dar Live kuwa Hip Hipo imeanzia Dar sio A-Town kama wasemavyo wao”.
Bonta amesema “kwakuwa kila mtu anauhuru wa kufanya au kuongea katika hii nchi basi acha awehuru, me sishangai anayosema yeye kwakuwa yuko huru kisheria hivyo muacheni aamue kujiita au kufanya analotaka, ila nachoona anataka kutafuta jina kupitia weusi”.
Kwa mujibu wa weusi na wakali wengine kutoka Lunduno wanasema Nicki Mbishi anaamua kujitafutia jina kwa kuwa anaona ameshapotea kwenye game la Hip Hop ndio maana anajaribu kukopi majina ya watu na kujipa yeye.
Mbali na hilo pia kuna Bifu la Afande Sele na Chid Benzi
Afande                                       Chidy
Sele almaarufu kama Mfalme Sele alisanuka kwenye mahojiano na kipindi kinachorushwa na channel five “FRIDAY NIGTH LIVE”, Sele amefunguka kuwa Ditto kuamua kujitoa Lafamilia na kujiunga na THT ni maamuzi sahii, kwani ni sawa na mcheza soka katoka Astorn Villa na kuamia Manchester United. Hata hivyo huyo mkuu wa La Familia “Chidy Benzi” tumemtunuku sisi kwani jina la Benzino kapewa na Professor Jay na tukaona tumfupishe tumuite Chidy Benzi, nikijana mdogo sana kwenye game enzi hizo sisi tunaimba yeye hata kuwaza kuimba hakuwaza sasa nashangaa leo anadiss wakongwe. Namuonya atapoatea asipotake care.
Chidy akafunguka kupitia mtandao wa facebook na twitter akiwa safarini kutokea Mtwara;
Kutoka facebook
Kutoka Twitter

No comments: