Monday, 20 February 2012

New Video: Mawazo by Diamond

Video ya wimbo Mawazo kutoka kwa msanii Diamond,
 ni kwamba ilikuwa inasubiriwa kwa hamu sana.
Kisa?Wakati wa kutengenezwa kwa video hii,
kiliibuka kitu ambacho baadae kilisababisha gumzo lingine.
Ilisemekana kwamba Diamond na Jokate
(miongoni mwa warembo wanaopamba video hii)
walionekana kuwa na ukaribu usio wa kawaida.
Wenye kujua mambo wakanadi kwamba wawili hao,
bila shaka walikuwa wameanzisha kajisafari ka mapenzi.
Moja jumlisha mbili ikawa kumi. Maneno yalipomfikia
Wema Sepetu(girlfriend wa Diamond kwa wakati huo)
kumi ikawa kumi na mbili na mwisho wa mapenzi yao
ukawa umeanza kujongea. Kipindi hicho hicho
Diamond akaachia wimbo mwingine akiuliza ampende
nani(song title:Nimpende Nani).Udaku ukashika moto.
Mengi yakaongelewa nk. Sasa ni wakati wa kuitazama
video yenyewe. Hii hapa chini.Binafsi  nimeipenda
hususani muonekano na quality yake. Pamoja na hayo
Diamond hajaonyesha kama ana mawazo kikweli.
Ukiwa na mawazo na ukiwa unatamani kunywa pombe,
bila shaka wajua inavyokuwa! Maudhui yamepotea kidogo.
Lakini kwa ujumla,it’s a good video.

No comments: