Ni yule kijana mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Juma Hassan Kaoneka, leo asubuhi amenitumia Email na kujitetea kuwa yeye sio tapeli kama ilivyoripotiwa na blog hii, bwana Juma ameumizwa sana na taarifa hizo za utapeli sababu zimemchafulia jina na hasa katika biashara zake..
Juma amesema "Kuna habari alizitoa Aziza Mkwata zinazonihusu mm Juma Hassan Kaoneka hizo habari si za kweli kabisa mimi ni mtu ninayejiheshimu kama ningekua nafanya hayo anayoyasema nisingekua huru na mambo yngu sijawahi kutapeli wala kumdhulumu mtu na watu wote niliofanya nao biashara na ninao fanya nao biashara nina mahusiano nao mazuri tu na kuwasiliana nao kama kawaida ila hili suala ni la kifamilia zaidi.."H ivyo basi anaomba wadau na jamaa zake wakaribu hususani wale aliokuwa anafanyanao biashara wasimfikirie vibaya.
No comments:
Post a Comment