Friday 9 December 2011

DR MWAKYEMBE IS BACK SOON FROM INDIA

 NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa kutoka nchini India alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi.

Dk Mwakyembe aliondoka nchini Oktoba 9 kwenda India kupata matibabu zaidi katika Hospitali ya Appolo, baada ya hali yake ya afya kuzorota.

Jana akizungumza kuhusu maendeleo ya afya ya mbunge huyo wa Kyela, Msemaji wa familia ya Mwakyembe na Mbunge wa Jimbo la Lupa,Victor Mwambalaswa, alisema Dk Mwakyembe atarudi nchini kabla ya Sikukuu ya Krismas na mwaka mpya.

Mwambalaswa alisema hadi jana hali ya afya ya Dk Mwakyembe ilikuwa ikiendelea vizuri na kuongeza kwamba ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa ngozi umepona, jambo ambalo limeonyesha matumaini. “Hali ya kiafya ya Dk Mwakyembe ni nzuri, hivyo wakati wowote kuanzia sasa, anaweza kurudi nyumbani (nchini), kuendelea na majukumu yake ya kikazi, jambo ambalo limeweza kutuletea matumaini,”alisema Mwambalaswa.

Aliongeza kwamba Dk Mwakyembe sasa anaendelea vizuri tofauti na wakati uliopita ambapo ngozi yake ilionekana kusinyaa. “Hali yake imerejea kama kawaida,” alisema. Mwambalaswa aliwataka Watanzania waendelee kumuombea Dk Mwakyembe ili aweze kujumuika nao katika kipindi cha sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya.

“Matibabu aliyopata nchini India yameweza kumsaidia kurudi katika hali yake ya kawaida, jambo ambalo tunaamini kuwa anaweza kuendelea na majukumu yake ya kitaifa.
Hivyo tunaomba wananchi waendelee kumwombea,”alisema Hali ya Dk Mwakyembe ilianza kubadilika mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, baada ya kuanza kuwashwa ngozi miezi michache iliyopita jambo ambalo lilisababisha kuvimba sehemu ya mwili wake.

Hali hiyo ilifanya alazimike kwenda nchini India kwa matibabu ambako alilazwa katika Hospitali ya Apolo akiendelea na matibabu kwa muda wote huo.

No comments: