Thursday 20 January 2011

CHIDY AMZINGUA BERRY BLACK

Msanii wa miondoko ya hip hop Bongo "Chiddy Benzino" hivi karibuni amesemekana kamtwanga makonde msanii mwenzie "Berry Black" kwenye club maarufu jijini Dar-es-salaam "Club Billcanas.
Inasemekana Chiddy alikereka na kitendo cha Berry Black kutomsalimia, hivyo basi akaamua kumfuata alipokuwa amekaa na kuanza kumzingua kwa matusi na ngumi kadhaa, kitendo hicho kilimpelekea Berry kukimbia kwa mabaunsa wa club hiyo.
Hata hivyo wasanii hao walifanya mahojiano live na mtangazaji wa Clouds Fm"B-12", Berry Black alieleza ilivyokuwa lakini Chidy alipopigiwa simu akazingua alivyopokea akasema ampigie baadae kidogo yupo kwenye mkutano na baadae akawa hapatikani tena hewani..Dizain kama chidy alijua kuwa yeye ndio mkosaji.


No comments: