Wednesday, 12 November 2014

R.I.P Geez Mabovu

Habari zilizotufikia usiku huu ni kwamba leo taifa limempoteza kijana mwingine mpiganaji wa 'game' ya bongo freva, "Hemed a.k.a Pengo" maarufu kama Geez Mabovu...
Kwa mujibu wa chanzo chetu bado hajatujuza nini hasa kimepelekea kifo cha msanii huyo...ila ametutumia Hash Tag (#) ya msanii mwenzie kutoka Tongwe Records maarufu kama Roma Tongwe akiwataarifu wadau kuhusiana na tukio hilo na kuweza kuwajibika kwenye kumpumzisha nguli huyo huko kwao mkoani Iringa.
Geez Mabovu ni miongoni mwa wasanii waliowahi kuwa washkaji wa karibu na msanii Albert Mangwea na kuweza kusaidiana kwenye harakati nyingi zikiwemo zile za kimuziki na za ishu zao binafsi.

Bwana ametoa na bwana ametwaa R.I.P Geez Mabovu...

No comments:

Post a Comment