Tuesday, 26 November 2013

Zanzibar yaialika China na Vetnam kwenye kombe la mapinduzi

Serikali ya Zanzibar yaialika China na Vetnam kuleta vilabu (timu) vyao kuja kucheza kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayotaraijiwa kufanyika na kumalizika mwanzoni mwa mwaka (January 12, 2014) ikiwa na lengo la kuazimisha miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Mualiko huo umetolewa mapema wiki hii na Makamu wa awamu ya Pili katika serikali ya Zanzibar, Balozi "Seif Ali Idd" ambaye pia ni Mwenyekiti wa "National Celebration Committee"...Amesema wameamua kuialika China na Vetnam kwa kuwa ni miongoni mwa nchi zilizoisapoti Zanzibar kwenye Mapinduzi mapema mwa 1964 baada ya kumalizika kwa utawala wa kikoloni.

Balozi Seif Ali ameziomba sana serikali za nchi hizo mbili kuweza kutoa support kwa vilabu vyao pindi vitakapokuwa vikicheza kwenye mashindano hayo yaliyogawanywa kufanyika katika kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itafanyika huko Pemba na ya pili kufanyika Unguja na mwisho kumalizikia katika viwanja ya Aman Stadium huko Zanzibar ikiwa ndio siku ya fainali.

Pia amewahakikishia kuwa serikali ya Zanzibar itawahudumia mahitaji mbalimbali kama usafiri na mahali pa mazoezi kwa timu zao zitakapokuwa zikijiandaa na pindi michezo hiyo itakapoanza, ila iliwaomba wao waweze kusafirisha timu zao kuja na kipindi mashindano yamemalizika.

Kwa mujibu wa mabalozi wa nchi hizo "Nguyen Thanh Nam - Vetnam na Lu Youging - China" wameahidi kufanyahivyo na kutoa support kwa vilabu vyao.

CHANZO: DAILY NEWS

No comments:

Post a Comment