Mkali wa Hip Hop kutoka nchini Marekani, Jay Z amepewa shutuma zilizodai kuwa ameiba wimbo wa "Run This Town". Inafahamika kuwa ni miaka minne sasa tangu kutoka kwa kibao hicho cha "Run This Town" alichofanya na mkali Kanye West pamoja na Rihanna. Jay Z ameshutumiwa na kampuni moja inayofahamika kwa jina la Tuf-America Inc kwa madai ya kutumia sampo ya wimbo huo. Wimbo huo uliofahamika kwa jina la "Hook & Sling" ulioimbwa na Eddie Bo, uliachiwa mnamo mwaka 1969 chini ya kampuni hiyo. Hata hivyo Jay Z pamoja na timu yake bado hawaja jibu lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
TIZAMA VIDEO YA WIMBO HUO
CHANZO: MTV BASE
inshu kama hzi zmezoeleka sana kwenye majna ya mastaa wa bongo kumad hata mbele noma sana
ReplyDelete