Saturday, 12 October 2013

Wahamiaji 16 kutoka Somalia wakamatwa ndani ya lori lililosheheni chokaa

Wahahamiaji 16 ambao ni raia wa Somalia wamekamatwa leo mkoani Morogoro wakitokea jijini DSM kuelekea mikoa ya kusini. Wahahamiaji hao walikamatwa wakiwa ndani ya lori lililosheheni chokaa maeneo ya Iringa road (Chamwino) mkoani Morogoro...kutokana na msaada wa wananchi pamoja na jeshi la polisi mkoani hapo vijana hao wapatao 16 walikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi kilichopo mkoani hapo.

Kwa mujibu afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro, Hamphrey Minja amesema kufuatia kuwepo kwa ulinzi mkali katika mipaka ya Tanzania kumewapelekea wahamiaji wengi haramu kutafuta njia mbadala za kuweza kuingia katika nchi hii ikiwemo hii ya kujificha kwenye magari ya mizigo.

Hta hivyo dereva wa gari hilo ametiwa nguvuni na jeshi la polisi pamoja na wahamiaji hao wapatao 16 ambao wengi walionekana kuchoka kufuatia kukosa hewa kwa muda mrefu na kukaa na njaa kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment