Thursday, 25 April 2013

mauwaji ya mwanafunzi wa chuo cha uhasibu Arusha

Jana majira ya saa sita mchana tulipokea ujumbe toka kwa mdau wa blog hii na kututaarifu kuwa Arusha kuna mgomo wa wanafunzi wa chuo cha uhasibu (IAA) na mgomo huo umepelekea kikosi cha usalama kulipua mabomu ya machozi ili kuweza kuwatawanya na kuzuia ghasia hizo za wanafunzi.
Sababu zilizowapelekea wanafunzi hao kugoma ni kufuatia kuuwawa kwa mwanafunzi mwenzao jana yake usiku majira ya saa nane na watu wasiojulikana. Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Henry Kago ni mwanafunzi wa chuo hicho cha IAA (Institute of Accountancy Arusha) aliuwawa kwa kuchomwa kisu na kujeruhiwa sehemu za shingoni na usoni na watu wasiojulikana akiwa anatoka chuo kujisomea na kurudi hostel alikokuwa anaishi.
Maiti ya Henry Koga baada ya kuuwawa
(tunaomba radhi kwa picha hii)
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za polisi zimeripoti kuwa hadi muda huu hawajajua sababu za kuuwawa kwa mwanafunzi huyo na pia hawajajua ni nani muhusika wa tukio hilo, ila wanaendelea na uchunguzi wa kina kwa tukio hilo.
post ya mmoja wa watu wake wa karibu 
walioonesha kuguswa na kuumizwa
 na kifo cha kijana huyo
Mh. Godbless Lema alikuwepo katika eneo la chuo hicho ili kuweza kuongea na wanafunzi hao kujaribu kutulia huku akiwaomba waache mgomo huo na kuliachia jeshi la polisi lifanye kazi yake.
Mh. Lema akijadiliana kitu huku akiongea na wanafunzi hao
Wanafunzi wakimsikiliza Mh. Lema na tamko
 toka kwa uongozi wa chuo
Matukio kama haya ya kuuwawa kwa wanafunzi hasa wa chuo yamekuwa yakitokea mara kwa mara hapa nchini, kama umekuwa na kumbukumbu mwanzoni mwa mwaka huu(2013) wanafunzi wa IFM walianzisha mgomo kwa tukio lililotokea kigamboni DSM baada ya kulawitiwa baadhi ya wanafunzi wa chuoni hapo na kuwepo kwa matendo ya uharifu kama kuporwa vitu vyao kama laptop, simu na fedha. Pia kulikuwepo kwa tukio kama hilo mkoani Dodoma kwa baadhi ya vyuo kama tunakumbuka mwanzoni mwa mwaka jana(2012), chuo cha St. John kulitokea mgomo wa wanafunzi uliosababishwa na tukio kama hilo la kuporwa bidhaa na fedha zao, kufanyiwa vitendo vya ulawiti na kuuwawa kwa wanafunzi. Mipango (IRDP) pia mwaka jana (2012) mwanzoni kulikuwepo na matukio ya ukabaji na uporaji wa bidhaa na fedha kwa wanafunzi.....

Je, kupitia jeshi la polisi serikali imeweka mikakati gani kuhakikisha matukio kama haya yanakomeshwa na kuchukuliwa hatua kwa wahusika wa matukio kama haya ya mauwaji hasa kwa wanafunzi wa vyuo??.

No comments:

Post a Comment