Saturday, 6 April 2013

Kingzila aamua kumtokea shabiki segerea


Msanii wa kizazi kipya nchini Tzee Godzilla aka Godzizi hivi karibuni amefunguka kuhusu mpango wake wa kushow love kwa kumtembelea moja ya shabiki wake mkubwa aliefungwa gereza la segerea.

Taarifa hizi zimeenea siku chache baada ya msanii wa filamu nchini maarufu kama Kajala kufunguka kupitia mahojiano ya kutuo kimoja cha radio kuwa wakati alipokuwa korokoroni gereza la segerea alipata nafasi ya kukutana na mtu mmoja anae mzimia msanii Godzilla to the maximum.

Mfungwa huyo alietajwa kwa jina moja la Zahara inasemekana ni shabiki namba moko wa Gozizi huko prizon ambae anaugua kukutana face to face na Rapper huyo one day.

Baada ya habari hizo kumfikia Gozilla Rapper huyo alifunguka bila kufikiria mara mbili kuwa anytime soon atatimba gereza la segerea ili kukutana na mfungwa huyo ambae ni shabiki mkubwa wa muziki wake.

Zilla amesema maamuzi yake yana lengo moja tu la kumpa shabiki wake haki ya kujiskia kuwa mziki unaweza kumuunganisha na mtu anaempenda akiongeza kuwa kufanya hivyo kutawezesha kuwafanya watu wengine kama Zahara kuamini kuwa zilla ni mtu wao.

No comments:

Post a Comment