Thursday, 28 March 2013

wema afanya tena kufulu

hawa ndio mbwa wa mwanadada huyo
Staa wa filamu za Kitanzania, Wema Isaac Sepetu baada ya kufanya kitendo kilichomuongezea umaarufu kwa wapenzi na mashabiki wa sanaa yake kwa kitendo cha kumtoa mwigizaji mwenzake "Kajala Masanja" kwa kuweza kumlipia pesa taslimu Tshs. million 13, hivi karibuni ameishangaza tena jamii kwa kile kitendo ambacho naweza sema ni cha kukufulu kwa kuwafanyia mbwa wake wawili (Vanny na Gucci) shopping iliyogharimu dola 4000 za kimarekani (zaidi ya shilingi milioni 6 na zaidi)…
Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao ''perfume'', viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri…
Akizungumzia ''shopping'' hiyo nyumbani kwake Kijitonyama, jijini hapa Dar, Wema alisema: ''Ki ukweli nawapenda sana hawa mbwa, ukinipasua roho yangu utawakuta, ndio maana nataka wavae na kunukia vizuri, kinyume chake siwezi kuwa na amani… najua watu wanaweza kushangazwa na kitendo cha mimi kutumia kiasi hicho cha fedha lakini sioni kama ni tatizo kwani ni kitu ambacho kinanipa furaha katika maisha yangu''…alifunguka mwanadadashosti huyo.
Jana mchana kupitia Instagram, Wema ameandika: ''Vanny ake heading to da hospital… my poor baby is sick… nat happy at all, hope u get better soon''

No comments:

Post a Comment