Friday, 27 July 2012

mr blue afunguka baada ya kupata mtoto

 
Wiki iliyopita msanii wa kizazi kipya nchini Herry Samir almaarufu kama Mr. Blue a.k.a Kabaisor alijaariwa kupata mtoto wa kiume aliyezaa na bibie Wahida Mohamed. Alimpa jina lake la Herry kwa kuwa ni mtoto wake wa kwanza. Bayser alisema hataki Herry awe maarufu, "namuomba mwenyezi mungu amjaalie Herry awe kiongozi ambaye ataweza kuwasaidia watu", alifunguka Mr. Blue alipokuwa akihojiwa na East Africa redio jana. Bysor ambaye kwa sasa anakamilisha mjengo wake wa kuweza kuitunza familia yake, alisema mungu akijaalia baada ya miaka miwili anaweza akawa ameimaliza nyumba hiyo.

No comments:

Post a Comment