Wednesday, 11 April 2012

MY BEST 10 MOVIES FROM THE LATE KANUMBA a.k.a THE GREAT

No.1: VILLAGE PASTOR
 Hii ndio ilinifanya nizidi kumkubali marehemu 
Steve Kanumba (THE GREAT)hasa vile alipocheza 
kusalitiwa na mkewe ambae ni Aunt Ezekiel na
 kutembea na rafiki yake mpenzi pia ni mchungaji 
mwenzie.
Hapa kanumba akijadili kitu na mkewe Aunt Ezekiel,
 ni moja ya sehemu kwenye filamu hiyo
No. 2: THE LOST TWINS
Movie ambayo aliigiza na Lucy mdada aliyeweza kucheza 
sehem mbili tofauti yaan ya kulwa na doto, 
ni moja ya filamu nilizozipenda na ntazidi zipenda
No. 3: CRAZY LOVE
 Hii huwa naipenda jinsi Kanumba alivyo'act kama chizi
 japokuwa story haijanifurahisha saaaana, ila
 The Great huwa ananikosha sana
 zile reference za authors anaowatumia
 No. 4: DEVIL KINGDOM
The devil Kingdom pia naipa namba 4 sababu
 imenipendezesha uwezo na idea aliyoitumia marehemu
Kanumba, ya kuweza kushawishiwa na wanaomuabudu
shetani na kuwa mmoja wapo
pia nimependa alivyoitendea haki Ramsey Noah
No. 5: MOSES
Hii nilipenda Kanumba alivyoeleza kisa cha kuwachukia
wanawake, na pale alivyocheza wema kuwa mvumilivu kwa
yote aliyotendewa na mumewe Kanumba,
yaan manyanyaso ya kila namna
No.6: RED VALENTINE
Ni filamu ambayo marehemu Kanumba amecheza
akimtesa sana mkewe Wema kwa kuwa hawajajaariwa
kupata mtoto, hivyo Kanumba anaamua kutembea na
mwanamke mwingine ambaye ni Jackline Wolper
Wema Sepetu akimshukuru Mungu baada ya kuambiwa ni 
mjamzito katika moja ya scene ya filamu hiyo
Doctor anawaelezea Steven Kanumba aliye'act
kama(Nicholaus) na Wema Sepetu (Vivian) kama
 mme na mke katika moja ya scene
sababu za mwanamke kutokushika mimba au sababu za
mwanaume kukosa uwezo wa kumpa mwanamke mimba.
No. 7: BIG DADDY
Aisee nimependa sana wale watoto walicheza kama
watoto wa Steve Kanumba, hasa kale katoto
kamwisho kame'act poa sana na ndio main
character kwenye hii movie. Pia Benny aliyeitwa
Selengo kwenye hii movie ambaye amecheza kama mlizi
wa nyumba ya hiyo familia ya Kanumba (Big Daddy)
No.8: MAGIC HOUSE
Nimevutiwa sana na story ya hii filamu, pia walioact
kama vile Benn aliyecheza kama mrithi wa hiyo
(Magic House) nyumba iliyoachwa na marehemu
ambaye ni Kanumba akiwa kama mmiliki wa
nyumba hiyo yenye masharti ya kila namna.
Nargis Mohamed, msichana aliyecheza kama mpangaji na
kisha kuinunua Magic House na kutokea kupendwa na
mmiliki ambaye ni mzimu S.Kanumba, nakubahatika
kuwa mke wa mzimu (Kanumba). Nae pia ameitendea
 haki hii filamu kwa kweli.
No.9:YOUNG BILLIONAIRE
Aisee humu jamaa wote walikamua sana, naweza
sema hii ndio filamu iliyomtambulisha bwana
Pancho Mwamba.
No.10: UNCLE JJ

Hizi ni sehemu ya movie hiyo ambayo Kanumba anajaribu
kumkanya mtoto aliyechezanae kwenye filamu hii akitumia
jina la Jeniffa

NAOMBA MNIELEWE KUWA HIZI NI ZILE NILIZOVUTIWA NAZO SAAAANA JAPO ZIPO FILAMU NYINGI SANA ZIKIWEMO JOHARI, WHITE MARIA, CROSS MY SIN,SHE IS MY SISTER, DAR TO LAGOS, DANGEROUS DESIRE NA ZINGINE NYIIIIIIIINGI ALIZOWAI KUCHEZA ALIYEKUWA MUIGIZAJI NGULI NCHINI MAREHEMU STEVEN KANUMBA.
HAKIKA TUTAKUKUMBUKA SANA KAKA, MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI,
EIMEN!!!

No comments: