Friday 12 July 2013

MAMA AMCHOMA MWANAE KWA MKASI MARA 90


Tukio hilo limetokea huko china baada ya mama kumchoma mwanae kwa mkasi mara 90 kwa madai kuwa alimng'ata ziwa akiwa anamnyonyesha.

Kwa mujibu wa Daily Mail mtoto huyo Xiao Bao mwenye umri wa miezi nane (8) ameshonwa zaidi ya nyuzi 100 ili kurudisha uso wake katika hali nzuri baada ya kufanyiwa kitendo hicho na mama yake mzazi.

Mtoto huyo (Xiao) ambae anaishi na mama yake mzazi na wajomba zake katika jiji la Xuzhou mashariki mwa China. Wajomba zake hao wawili ambao wanajishughulisha na ukusanyaji wa taka kwa kujipatia kipato.

Mmoja wa wajomba hao ndiye aliyegundua tukio hilo baada ya kumkuta mtoto huyo (Xiao) akiwa amelala katika damu zilizotapakaa nyumbani hapo.

Mama mzazi wa mtoto huyo baadae alikiri kitendo hicho cha kumchoma mwanae kwa kutumia mkasi mara 90 katika eneo la uso baada ya kumng'ata wakati akimnyonyesha.

Baada ya tukio hilo majirani waliiomba serikali ya nchini humo kumnyang'anya mtoto huyo lakini serikali ilitupilia mbali maombi hayo kwani hadi sasa hawajapata kufahamu kuwa mama huyo ana matatizo ya akili au lah. Pia wamesema kwa kuwa mtoto huyo bado anauwezo wa kuendelea kupata malezi kutoka kwa wajomba zake hao.

Mbaka sasa mtoto huyo bado anaendelea na matibabu akiwa Hospital.

1 comment:

Unknown said...

sio mzima huyo mama